Kaa tayari kwa Ujio wa Nikki Mbishi akiwashirikisha Lady Jay Dee, One Incredible na Songa 'kupanda na Kushuka'

Rapper wa Tamaduni Muzik, Nikki Mbishi anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Kupanda na Kushuka’ aliowashirikisha Lady Jaydee, Songa na One the Incredible.Nikki amesema ameamua kuwashirikisha wasanii hao ili kupata kitu tofauti kama muziki unavyohitaji.




“Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani fulani ili uwe mzuri zaidi na hii ni kawaida ya muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu kwa pamoja kitakuwa safi tukaingia studio za Man Walter tukafanya wimbo ‘Kupanda na Kushuka’, ni wimbo ambao unaelezea maisha ya kawaida kupanda na kushuka kwa maisha, leo umepata kesho umelala njaa lakini ni maisha. Wimbo utatoka hivi karibuni pamoja na video,” alisema Mbishi.
Previous Post Next Post

Popular Items