Jk Nyerere airport ipo katika orodha ya viwanja vibovu vya ndege afrika

Afrika ina heshima ya kuwa na baadhi ya viwanja vya ndege ovyo duniani na, tukiwa wakweli, ni rahisi kuona kwanini.

Katika tafiti za mwaka huu, wapigakura walikuwa tayari kutuma habari zinazohusiana na viwanja vya ndege vibaya katika bara hilo.



Kuanzia sakafu chafu na vyoo vichafu pamoja na kuomba rushwa, wasafiri walikerwa na viwanja vya ndege ambavyo viliingia katika orodha ya Viwanja Ovyo barani Afrika.

Malalamiko mengine ni kukosekana na vitoa hewa baridi (air-conditions) katika hali ya joto, msongamano, migahawa duni na usalama wenye maswali kibao yasiyo tija.

Ikiwa unasafiri kwenye viwanja hivi, watu wengi hukimbia sehemu za kulala za viwanja hivyo hata pamoja na nyumba za kulala zilizopo karibu na maeneo ya viwanja.


Hii ni orodha ya Viwanja vya Ndege Ovyo vilivyopatikana kwa mujibu wa wapigakura kwenye Tafiti ya Viwanja vya Ndege 2014.

  1. Khartoum International Airport, Sudan (KRT)
  2. Kinshasa N’djili International Airport, Democratic Republic of the Congo (FIH)
  3. Tripoli International Airport, Libya (TIP)
  4. Dar es Salaam Julius Nyerere International Airport, Tanzania (DAR)
  5. Luanda Quatro de Fevereiro International Airport, Angola (LAD)
  6. Port Harcourt International Airport, Nigeria (PHC)
  7. Abuja Nnamdi Azikiwe International Airport, Nigeria (ABV)
  8. N’Djamena International Airport, Chad (NDJ)
  9. Accra Kotoka International Airport, Ghana (ACC)
  10. Lagos Murtala Muhammed International Airport, Nigeria (LOS)
Hatahivyo, terminal mpya inajengwa kwenye Uwanja wa Ndege Dar es Salaam ambapo ukiisha, utaifanya Dar kuwa na uwanja unaokubalika kimataifa.

Previous Post Next Post