Hot: Martin Kadinda baada ya kumpatia Wema BMW kwenye birthday yake, afunguka na kusema haya 'Wema deserve good thing'

Manager na mbunifu wa mavazi Martin Kadinda amefunguka na kuzungumzia zawadi ya gari aina ya BMW aliyomkabidhi Wema Sepetu kama zawadi ya siku ya kuzaliwa, katika sherehe ilizokafanyika siku ya Jumapili September 28 nyumbani kwa mwanadada huyo.



Wema Sepetu akikabidhiwa kadi ya gari hiyo

Martin amesema gari alilomkabidhi Wema ni michango ya wadau mbalimbali ambao wanam-support mwanadada huyo.

“Wema deserve good thing, mimi kumpa zawadi bi dada, waliokuwepo kwenye party wamesikia sikusema mimi ndo nimenunua, nimesema nimetoa nilichokuwa nacho, na nimepita kwa watu walichokuwanacho ambao wanasimama kwajili ya Wema. Kuna watu kibao wanasimama kwajili ya Wema, kwa mfano kama Bongo61 wanamsapoti Wema either yupo chini au juu, kwahiyo nimepita kwa watu ambao wamekuwa wakim-support Wema, watu ambao wakiniona nipo chini wananiambia Martin simama fanya hivi, vitu vingi vilivyokuwa vinafanyika pale watu wengi walikuwa wanajitolea, huyu kajitolea hiki yule kajitolea hiki.

When comes kwenye gari nilipita kwa watu, they can support me hata nikiwa sina chochote nikaweza kukusanya, pia Wema hakai bure Wema anafanya kazi, kila siku unasikia Wema kaenda kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli fulani, kila kitu alichokuwa ananipa mimi nilikuwa na save ili nimuonyeshe Wema tukiamua kukaa chini na ku save money , tutafanya vitu vikubwa zaidi ya hivi ulivyoviona, mimi mtu wa pembeni yako nimeweza ku–afford kukusanya pesa ukapata gari yako, kwa nini usikae ukatunza vile ulivyonavyo na ukafanya vitu vikubwa zaidi, kwahiyo nimempa kama challenge ya kumfanya ajue kwamba kuna watu wa pembeni yake wana make more money kwa kutumia jina lake na yeye hajui, kwaiyo imemuonyesha kwamba if you seat down aamue sasa napiga kazi you will be much millionaire, kwaiyo kama kuna watu wanaweza wakakaa pembeni na wakani-support mimi manager wake, je yeye akiamua kuwafuata front akawaambia jamani nataka hiki na hiki inashindikana? Kwahiyo the reason behind Wema anatakiwa kusimama” alisema Martin




BMW ya Wema

Pia Martin amekanusha kuwa hawafahamu hao mabwana ambao wanadaiwa kuhusishwa kwenye ununuzi wa gari hiyo.

“Sijui eti gari ni mkongo mpaka sasa hivi wametajwa watu zaidi ya hamsini, sasa sijui ni yupi ambao wao wanasema katoa gari, sijawai kumfahamu mkongo wowote katika maisha yangu kwa Wema never, sijawai kuonana nae sijui rafiki yake wa TRA never, kwahiyo hao watu ambao wanazusha hayo maneno hahisi ni wapinzani wake ambao hawapendi kuona Wema aendelea ni bora hata wangeungana kuliko kutoa story zaidi ya ishirini maana kila mtu ana story yake, kwaiyo watahangaika tu mwisho wa siku Wema ndo mmiliki wa gari, ndo kapewa na Martin Kadinda watake wasitake lakini ukweli ndo huo,” alimalizia Martin.
Previous Post Next Post