Diamond Platnumz apewa dili nyingine na waziri huyu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu amemtunuku msanii wa muziki wa kizazi Kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’, kuwa balozi wa utalii katika upande wa sanaa.

Akizungumza jijini hivi karibuni, Waziri huyo alisema mikakati ya kuandaa mikataba ambayo wataingia na msanii huyo imeanza.


“Wewe ni moja kati ya watu ambao wamekuwa wakijitahidi kuitangaza nchi yetu kimataifa, unastaili kuwa balozi na kuendelea kulitangaza taifa letu,”alisema Nyalandu.

Kwa upande wake Diamond alishukuru kupewa nafasi hiyo na kuhahidi kuitendea haki ya kuitangaza zaidi Tanzania.
Previous Post Next Post