Video: Nando yupo tayari kumuoa Lulu sasbau ni wife material

Ammy Nando na Lulu walitengeneza vichwa vya habari mara kadhaa wakihisiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi. Hata hivyo wawili hao kwa nyakati tofauti waliueleza uhusiano wao kuwa ni wa kirafiki.

Lakini Nando bado anamuangalia Lulu kwa jicho la tatu kama wife material.

Ammy Nando amefunguka kuwa yupo tayari kumuoa Staa wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' maana ni 'wife material'.


Amesema Lulu ni rafiki yake, lakini ni msichana ambaye anamzimia kwa kuwa anajua kutafuta pesa japo ana umri mdogo.

“Lulu ni mwanaharakati, ni mdogo lakini she knows how to get money.” Amesema Nando.

Aongeza kuwa kutokana na sifa alizonazo za kutafuta pesa pamoja na uzuri wake, atakapokuwa na mpango wa kuolewa yeye yuko tayari kutulia nae.

Tazama interview aliyofanyiwa na Globa Publishers 


Previous Post Next Post