Video: Beyonce na Jay Z wakosolewa vikali, wadaiwa kuhamasisha uhalifu kwa filamu fupi wanazotoa

Beyonce na Jay Z wameendelea kuachia vipande vya filamu zinazowaonesha wakiwa katika harakati mbalimbali zinazohusisha matumizi ya silaha. Hivi karibuni wameachia filamu fupi ya ‘Bang Bang’ ya aina hiyo.

‘Bang Bang’ iliyoongozwa na Dikayla Rimmasch ikiwa na taswira ya Bonnie & Clyde inawaonesha wakifanya matukio ambayo yako kinyume na sheria. Baadhi ya vipande vilioneshwa kwenye wakati wakiwa jukwaani kwenye ‘On The Run Tour’.

Pia ilikuwa ikioneshwa kama sehemu ya trailer ya filamu itakayooneshwa na HBO September 20 na katika maonesho huko New York, Clic Gallery, September 19.



Hata hivyo, mtandao wa fishwrapper umeikosoa hatua ya Beyonce na Jay Z na kudai kuwa wanafanya upuuzi na kuhamasisha matumizi mabaya ya silaha na uhalifu katika jamii.

Umewataka wanamuziki hao kujikita katika kitu ambacho jamii inahitaji kama muziki wao na kwamba kwa kuwa wanaona kila wanachotoa kinapokelewa vizuri na mashabiki wanaowapenda sana, wasichukulie hiyo kuwa tiketi ya kuilisha jamii vitu visivyo na maana.



Hii ni sehemu ya maelezo ya mtandao huo:

“Why do Beyonce and Jay Z have to make short films about guns and crime and other such ridiculousness? Does anybody honestly care? If they went through the effort of making this film, why not just do something people care about and make more music? Are there actually people that do care about this? Do they think that highly of themselves that they believe they can do anything at all and people will worship it? What's next, a short film of Beyonce brushing her teeth? Seriously though, why not just make some music instead of waving around guns and promoting crime in an "artsy," "cool" way? WHY?”
Previous Post Next Post

Popular Items