Video: August Alsina azimia na kuanguka jukwaani wakati akitoa burudani 'Watch Video'

Hit maker wa ngoma ya No Love aliyomshirikisha Nick Minaj, August Alsina alijikuta akipata vifafa vya hapa na pale baada ya kuanguka wakati akitumbuiza jukwaani saa 24 zilizopita. Bado ameendelea kulazwa hospitali.




Mwakilishi wa msanii huyo ameuambia mtandao wa TMZ kuwa msanii huyo amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi jijini New York na anapewa matibabu ya kifafa. Alsina alizimia na kuanguka wakati akitumbuiza usiku wa jana jijini humo.



Amesema madaktari hawakukuta dawa zozote kwenye mwili wake zaidi ya bangi kwenye mfumo wake. Wanaamini kuzimia kwake kulitokana na kuchoka na kukosa maji.
Previous Post Next Post