Tailor Swift akumbwa na tishio la bomu uwanja wa Ndege, London

Mwanamuziki Taylor Swift alikuwa mmoja kati ya maelfu ya abiria waliokubwa na tishio la bomu katika uwanja wa ndege Luton, London, Uingereza, Jumatatu.

Mwanamuziki huyo alijikuta akiwa kati ya abiria wanaokimbia tishio hilo ambapo alifanikiwa kupanda ndege yake binafsi na kuondoka katika eneo hilo.



Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun kuwa kilimshuhudia mwimbaji huyo katika harakati za kukimbia na kupanda rangerover nyeusi iliyomfikisha kwenye ndege.

“It had somehow managed to navigate its way to a closed airport and Swift was able to board her flight.” Kilieleza chanzo hicho.

Tishio hilo liliripotiwa polisi na abiria mmoja baada ya kuona kuna mtu ana mfuko wa vitu vinavyotoa mvuke.

Polisi walitumia robot maalum kuupekua mfuko huo na mwisho wakagundua mtu huyo alikuwa na vifaa vya kutengeneza nywele na sio bomu kama ilivyodhaniwa.

Hata hivyo, tayari baadhi ya ndege zilikuwa zimeahirisha safari na nyingine kubadili muelekeo hali iliyowaathiri abiria hao.
Previous Post Next Post