Siwezi kuwasahau watoto yatima 'Odama'

Mwanadada kutokakatika kiwanda cha Bongo Movie Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa katika maisha yake hawezi kuwasahau watoto yatima na kuanzia sasa, kila mwaka lazima asherehekee nao katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.


Odama ambaye hivi karibuni alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kutoa misaada ya vyakula na vitenge kwa watoto yatima na walezi wao wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar huku akiangusha sherehe ya nguvu ndani ya ukumbi wa Vijana na kuungana na watoto hao, alisema huu ni wakati wa watoto kufurahi naye.



“Nimeshasherekea sana bethdei baa na marafiki zangu, lakini kwa sasa nimebadilika na ndiyo nimeanza mwaka huu nitakuwa na watoto yatima kila mwaka nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwani kama hivi wamejisikia faraja sana kuja kula pamoja na mimi, kucheza muziki pia kuwaona waigizaji mbalimbali imekuwa ni furaha kwao,”alisema Odama


Watoto yatima wakiwa katika picha ya Pamoja na Odama
Previous Post Next Post