Rapper Izzo Business aweka wazi kiasi alichototumia kushoot video ya Walala Hoi , aliyoishoot na Adam Juma

Rapper kutoka Mbeya, Izzo Bizness, amesema video ya wimbo wake ‘Walalahoi’ imetumia kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 4 peke yake.



Akizungumza na Enewz ya EATV, Izzo amesema video imechelewa kukamalika kwa sababu muongozaji wake amekuwa na kazi zingine nyingi wakati huu.

“Kuna vipande vichache tu vimebaki kwa sababu nyimbo yenyewe unaiona ilivyo, tumeongea mambo mengi, na sio muda ambao unahitaji kushoot unashoot tu. Unaweza ukahitaji kushoot director ana kazi nyingine tatu, nne kwahiyo unasogezwa mbele. Ndio maana imechelewa. Pia watu wategemee video kali kabisa. Video ni milioni 1 na laki 4 na Nick hapo tumemlipa kila kitu,” alisema Izzo.
Previous Post Next Post