Promota Huyu afunguka na kusema Alikiba anakubalika zaidi uingereza kuliko hata Diamond Platnumz

Promota wa muziki na filamu anayefanyia kazi nchini Uingereza, Hadija Seif maarufu kama Dida Fashion amesema wapenzi wa muziki nchini Uingereza wanampenda zaidi Alikiba kuliko Diamond.



Dida alisema hayo kwenye mahojiano aliyofanyiwa na tovuti ya Bongo5 hivi karibuni. “Sio sasa hivi tu, tangu zamani to be honest kwa UK Alikiba yupo juu zaidi,” alisema.




“Sijui kwanini lakini kwa watu wenyewe ukisema labda kati ya Alikiba na Diamond hapo nani aletwe, honestly watu wa UK yaani Alikiba sijui aliwafanya nini lakini Alikiba UK is the best,” aliongeza.
Previous Post Next Post