Picha: Dk. Mwakyembe azindua magari ya taxi ya mil. 840, JK Nyerere International Airport

Moja ya magari yaliyozinduliwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe leo makao makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ikiwa ni sehemu ya magari 54 yenye thamani ya sh. milioni 840 yaliyonunuliwa na Chama cha Madereva taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa mkopo kutoka Equity Bank kuboresha usafiri.

Baadhi ya madereva wa taxi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa magari yao wakifuatilia hotuba ya Waziri Mwakyembe. Kwa mbali kulia ni magari yao yaliyozinduliwa.


Waziri Mwakyembe, Mkurugenzi wa kiwanja cha JNIA, Bw. Moses Malaki (katikati)na Katibu wa Chama cha Madereva taxi, Antipas George Missana ( wa pili kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari hayo.

Waziri Mwakyembe, Mkurugenzi wa kiwanja cha JNIA, Bw. Moses Malaki (katikati)na Katibu wa Chama cha Madereva taxi, Antipas George Missana (wa pili kushoto) wakikata utepe.

Waziri Mwakyembe akiingia katika moja ya magari aliyoyazindua tayari kuendeshwa.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanachama wa Chama cha Ushirika cha Madereva taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo mchana makao makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Terminal I, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA, Bw. Moses Malaki.
Previous Post Next Post

Popular Items