Music : Pathogen feat. Chris Brown- Lady in A Glass Dress

Skywalker ameachia wimbo mpya unaoutambulisha pia jina lake jipya kwenye muziki ‘Music Pathogen’, wimbo ambao ameeleza kuwa chimbuko lake ni albam mpya ya Chris Brown ‘X’ na idea aliyowahi kuwa nayo miaka iliyopita.

“Lady In A Glass Dress ni interlude kwenye album mpya ya Chris 'X'. Japo ni fupi lakini ndio kipande ninachokisikiliza zaidi kwenye album hii.Ujumbe wake unafanana na mashairi niliyoandika miaka miwili iliyopita ya wimbo nilioupa jina 'Be Your Man' ambao sikuwahi kuufanya.” Amesema Skywalker katika maelezo yake.




“Nilichofanya nimeproduce beat mpya kwa kufuata ala za 'Lady In A Glass Dress' na kurekodi mashairi yaliyochanganywa na interlude hiyo. Nilipenda sana interlude hiyo 'Lady In A Glass Dress' iwe wimbo kamili so nimetimiza ndoto yangu ya kuufanya kuwa wimbo uliokamilika.” Ameongeza.
Previous Post Next Post