Hasheem Thabeet anunuliwa na Philadelphia 76ers huenda akahamia timu ya Cleveland Cavaliers

Kuna tetesi kuwa mchezaji wa Tanzania kwenye ligi ya mpira wa kikapu Marekani, NBA, Hasheem Thabeet anaweza kuhamia kwenye timu ya kikapu ya Cleveland Cavaliers baada ya kununuliwa na Philadelphia 76ers kutoka Oklahoma City Thunder.



Kwa mujibu wa ESPN, pamoja na Philadelphia 76ers kumnunua Thabeet kutoka OKC watamwacha kuwa huru na hivyo Cavaliers kumchukua kwa gharama nafuu.

ESPN wamedai Cleveland wanauhitaji mkubwa wa mchezaji wa kati, nafasi ambayo Thabeet anaimudu na hivyo kuwa msaada kwao.

“Nothing is certain, but Thabeet makes a lot of sense for the Cavaliers and is worth a shot at the minimum. He fills a need, comes cheap and would be someone that makes the frontcourt in Cleveland even more intriguing entering the season,” umeandika mtandao huo.

Thabeet amecheza kwenye ligi hiyo kwa misimu mitano.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA