Fahamu sababu wazitoazo wanawake wakitaka kukutosa ?

Unawea kuwa umeshaambiwa haya ila hata bila kujijua masikini ya mungu, bado mtu unakuta unang’ang’ania. Wadada wengi hukuta kipindi wanapokutana nawe na hata wakati ndio kwanza mnaanza mahusiano yenu, hukupima na kukuona kama unafaa, sababu unakuta labda hata mara ya kwanza kabisa anakuwa na juhudi za kutaka kukujua zaidi, ila mara nyingi mwisho wa siku anaona hakuna lolote hapo, ndio inapelekea kuchukua uamuzi wa kuanza kujitoa mdogo mdogo na hata mara nyingine kukufanya uwe rafiki tu,na hata mara nyingine kama ndio ulikuwa ujatupa madini, unaona huo ndio mda sasa wakutupia, ila usikiapo sentensi kama hizi..kimbia tu kiroho safi.





Tatizo siyo wewe, tatizo ni mimi, unastahili mwanamke bora zaidi yangu.


Maneno haya yana madhumuni ya kutokuumiza, zaidi ni kukufanya uendelee kujisikia vizuri huku ukiachwa, na mara nyingi unaweza kujua kuwa tatizo lipo kwa mwanamke mwenyewe, na mwisho wa siku unaona bora tu kumuacha aende. Hii ni moja ya ujanja wa zamani sana, wanawake hutumia hadi hii leo, ukweli ni kwamba, usikiapo umeambiwa hivi ujue “tatizo lipo kwako” huna alichokuwa anatarajia kutoka kwako, hapo ndio mwisho tena wa mkataba wa kukujua.



Sipo teyari kujingiza katika mahusiano kwa sasa


Kwa mtu asemayo haya, asingekuwa na wewe hata hapo mwanzoni, kujaribu kutaka kuwa rafiki yako huku akionyesha ishara na dalili zote za kutaka kuwa na wewe. Mstari huu unamaanisha haswa mahusiano hayo ya mwanzo kabisa mliokuwa nayo, hakutegemea kabisa kama yangekuwa hivyo, kwa hiyo anapokwambia hivyo ujue ameshatemana na wewe. Kama mtu kweli asingekuwa teyari kuingia katika mahusiano, angekwambia kabisa hapo mwanzo, siyo kukutega alafu mwisho wa siku ndiyo itokee kama haya.



Niko bize sana , sina muda hivi sasa wakujihusisha na mambo ya mahusiano.

Kama unampenda mtu, siku zote hutafuta muda hata wakuibia ukiwa kazini kutaka kuongea naye, angalau hata kuulizia kama anaendeleaje, na mara nyingi huwa na hamu kabisa ya kumaliza siku yako ya ubize ili kumuona mpenzi wako. sasa wakati mpenzi wako anapokwambia kwamba yuko busy, ina maana hakuchukulia serious kivile au simply not worth being taken seriously..



Nadhani sipo teyari kuanza kujihusisha na mahusiano kwa sasa.

Wanasema mahusiano ndio sehemu ya kwanza kuweza kujitambua kama upo tayari au la, hakuna asiyetamani kuwa na mpenzi au mtu anayemjali siku zote, mnaweza kuwa na uhusiano wa kuanza wa kawaida tu, muwe mnaongea mambo mbalimbali kuhusiana na maisha, kazi na malengo yako, wakati huo huo mkiendelea kuzoeana katika kujaribu kuingia katika next level, sasa ikifika mpenzi wako anakuomba nafasi yakutaka kufanya mambo yake, huu unakuwa ni ujanja tu wakutaka kujitoa katika mahusano yenu.
Previous Post Next Post