Al-Qaeda yatoa tangazo jipya kuhusu himaya yao na mpango wao

Wakati ambapo dunia inaendelea kuumizwa na vitendo vya kigaidi na kufanya jitihada mbalimbali za kukomesha, kiongozi wa kundi la kigaidi la Al- Qaeda, Ayman Al-Zawahiri ametoa tangazo kuwa kundi hilo limefungua tawi jipya nchini India.


Pichani: Al-zawahiri na Osama (enzi za uhai wake)

Kwa kujibu wa BBC, katika tangazo hilo lilitolewa kupitia kipande cha video linaeleza kuwa nia ya kuanzisha tawi hilo ni kutaka kuhakikisha wanapandisha bendera za Jihad kusini mwa bara la Asia kama walivyoweza katika maeneo kadhaa nchini Iraq na Syria kupitia kundi la ISIS.

Tangazo hilo linakuja ikiwa siku mbili baada ya majeshi ya Marekani kueleza kuwa yamefanya mashambulizi ya kushitukiza dhidi ya kundi la Al-Shabaab ambalo ni washirika wa Al-Qaeda na inawezekana lilisababisha kifo cha kiongozi mkuu wa kundi hilo ambaye yuko katika orodha ya watu 8 wanaotafutwa zaidi duniani na Marekani.

Hata hivyo, Marekani ilisema inafanya uchunguzi kufahamu kama walimuua kiongozi huyo ambaye hata picha yake haijawahi kuonekana.
Previous Post Next Post