Ubaguzi: Pub ya Korea Kusini yapiga marufuku wateja Waafrika kwa kuhofia Ebola

Katika hali isiyo ya kawaida, Pub moja nchini Korea Kusini imewazuia watu wote wenye asili ya Afrika kuingia katika Pub hiyo kwa madai kuwa wameamua hivyo kwa lengo la kujikinga na ugonjwa wa Ebola.

Tangazo hilo limezua hisia nyingi za kibaguzi na kusababisha baadhi ya watu kuitisha maandamano siku iliyofuata na kupanga kuingia kwa nguvu katika pub hiyo.




“Tunaomba radhi, kutokana na virusi vya Ebola haturuhusu waafrika kwa muda huu.” Linaeleza tangazo lililobandikwa katika Pub hiyo.

Taarifa nyingine zinaeleza kuwa kuna baadhi ya migahawa pia imepiga marufuku waafrika kwa hofu ya kupata maambukizi ya Ebola.

Hata hivyo, hakuna dalili zozote za kuwepo kwa maambukizi ya Ebola katika nchi hiyo kwa mujibu wa maafisa na kwamba ubaguzi huo unafanywa na watu binafsi na sio nchi.
Previous Post Next Post