Sean Kingston ashitakiwa na sonara kwa utapeli

Mwanamuziki Sean Kingston amefunguliwa mashitaka na sonara anaedai kuwa mwimbaji huyo amekuwa akimpiga danadana kuhusu malipo ya vidani na mikufu aliyomkopesha kati ya mwaka 2008 na 2013.


Sonara huyo aliyetajwa kwa jina la Avi Da Jeweler ameeleza kuwa alimkopesha Sean Kingston pete yenye thamani ya $16,000 ili atoke nayo kwenye kipindi cha 106 & Park lakini mwimbaji huyo hakurejesha kama walivyokubaliana.

Avi ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka kadhaa, mwimbaji huyo amemuandikia checks takribani saba lakini zote zilikataliwa.

Avi Da Jeweler anadai malipo ya $226,200 kama gharaza za vidani na mikufu hiyo na pia fidia ya $1 million kutokana na usumbufu alioupata.
Previous Post Next Post