Picha: Ay ndani ya White House ya Marekani, akiwa na wasanii wengine

Msanii kutoka aTanzania AY, ameungana wasanii wengine wakubwa barani Afrika jijini Washington DC, kwa mwaliko kutoka ikulu ya Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika utakaofanyika wiki hii.



AY akiwa White House

Wasanii hao ni sehemu ya wale walioshiriki kwenye mradi wa One Campaign. Wasanii wengine waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Femi Kuti, Owamumi na D’Banj wa Nigeria, wa Afrika Kusini na Fally Ipupa wa DRC, Victoria Kimani wa Kenya, watakaoungana na mchezaji Manchester City, Yaya Toure mjini Washington D.C. kuanzia August 4-7.




AY akiwa pamoja na Femi Kuti, Victoria Kimani na wengine

Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka barani Afrika kwenye mji huo mkuu wa Marekani katika mkutano wa siku tatu. Huo ni mkutano mkubwa zaidi kuwahi kufanyika kati ya Rais wa Marekani na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali za Afrika.



@AYTanzania

AY Akiwa na Dbanj

@AyTanzania akiwa na  @adams_vj #WashingtonDC #SoundCityTv

Kwenye ziara hiyo, wasanii hao watakutana na viongozi wa juu wa serikali Marekani, wajumbe wa taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) na wajumbe wa Congress. Pia watatumbuiza siku ya August 4 ukiwemo wimbo wao wa ‘Cocoa Na Chocolate’.
Previous Post Next Post