Picha: Akon akutana na Rais Uhuru Marekani

Supastaa wa muziki mwenye asili ya Afrika, Akon ambaye makazi yake ni huko nchini Marekani, amepata nafasi ya kukutana na Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta na kuzungumza naye kuhusiana na mambo mbalimbali.



Kufuatia mkutano huo na Rais Kenyatta, Akon ameweka wazi kuwa kiongozi huyu amekuwa na maono makubwa kwa Kenya na kuahidi kutua nchini humo mwezi Septemba kwaajili ya kutekeleza baadhi ya maono hayo.

Nafasi hii ya kipekee imetokea wakati huu ambapo Rais Kenyatta amekuwa huko Marekani kwa ajili ya mkutano mkubwa wa Wakuu wa nchi za Afrika na Rais Obama.
Previous Post Next Post