Lady Jaydee ajibu tetesi za kuachana na Gadner kwa picha hii

Wanasema picha huongea maneno 1,000. Baada ya kuendelea kwa uvumi kuwa ndoa ya Lady Jaydee na Gadner G Habash imevunjika, muimbaji huyo amepost picha akionesha pete ya ndoa kwenye kidole chake.



Kupitia ukurasa wake wa Facebook wa Lady Jaydee ameandika ujumba tofauti na picha lakini mashabiki wake wameelewa kuwa ni ujumbe anaoutoa kufuatia tetesi hizo. “Kucha zimekosa rangi ya OriFlame tu, ili zing’ae zaidi ya hapo,” ameandika Lady Jaydee.



Soma baadhi ya ujumbe kutoka kwa mashabiki wake.
Anna Julius
Tetea ndoa yako dada, achana na maneno ya wa2.
Calvin Mpoto 
Jibu la magazeti ya bongo! Hongera J hayo ni mapito tu,kelele za chura hasishindi tembo kunywa maji!
Devotha Kyaruzi
Anamaanisha ndoa yake ipo acheni udaku.she is mrs gadner jamani oneni pete yake ya ndoa.
Previous Post Next Post