Hot: Adam Juma aeleza kwanini video nyingi za Bongo hazipigwi kwenye TV za nje

Mjadala wa kuhusu wasanii wengi wa Tanzania kwenda kufanya video zao nje ilhali tunao madirector wazuri nchini, na video zinazofanywa na madirector wa Bongo kutochezwa na vituo vya kimataifa umekuwa ukiendelea kila kukicha, huku kila mmoja akitoa mtazamo wake wa sababu ya wasanii wengi kukimbilia nje au video za kibongo kutochezwa na TV za kimataifa.



Adam Juma wa Visual Lab: Next Level ambaye ni mwongozaji na mtayarishaji wa video wa Tanzania, amezungumzia mambo kadhaa na kujibu maswali ya kwanini video nyingi za Bongo hazifiki au hazichezwi kwenye TV za nje.

TATIZO HASA NI NINI?
Kila mtu anaweza kusema anavyotaka kusema kwa uelewa wake, dunia ya sasa imebadilika lazima tukubali hilo. Huwezi kuongea uongo mbele ya umma halafu usibainike kama ni uongo au ukweli. Muziki wetu Tanzania una mapungufu mengi sana ila naona watu wanawalaumu madirector bila kuzingatia misingi ya kazi za hao madirector.
Kwani kazi ya director ni ipi? Majukumu yake ni yapi? Na je mmekubaliana nini kwenye kazi?


Ukipata majibu ya haya basi ni rahisi sana kujua kwanini video hazifiki kwenye TV za nje.

Kwanza kabisa kila msanii ajitambue na aelewe muziki anaofanya na unalenga wapi. Pili unaweza kufanya video kokote duniani huku ukizingatia vigezo ambavyo TV zote zinakubali, vigezo kama kujaza form husika na kufuata maelekezo ya wapi video itumwe au kupelekwa. Suala la kuzingatia pia TV station hizi zina uwezo wakuamua kutokupiga kazi yako kama hujatimizi maelekezo hayo au kama hawajairidhia kazi yako.

Kazi ya kujaza form ya video ni ya msanii au management ya msanii, kama ikitokea msanii anahitaji msaada wa kujaza basi anaweza kusaidiana na director ili kupeleka video. Kazi hii sio ndogo kama unataka kupeleka Trace, Channel O, MTV Base, BET, Soundcity, na nyingine, lazima uwe na internet yakuweza kuupload file la HD lenye 50mbp file size usiopungua 1gb kutumia dropbox au wetransfer.com . Hatua zote hizi zinatumia muda na gharama ambazo mara nyingi wasanii hawapo tayari kutoa ukiwaambia.
Sababu za video kukataliwa TV za nje

Kuna vitu vinachangia sana kufanya video isikubaliwe, vitu kama make up artist mzuri, ukimwambia msanii amlipe makeup artist laki 2 hataki anataka afutwe na poda, tena atajifuta mwenyewe, lighting kumpata gaffer mzuri na light za kutosha ni gharama ambayo wengi wanakimbia, kwa miaka mingi nimekua nikiziba mapengo haya, naplay role ya DOP and director sababu budget haitoshi kuzigawa hizi nafasi mbili.

Kazi ya director ni ipi?

Najibu swali la awali, kazi ya director ni kuiongoza video yote mwanzo mpaka mwisho, kuchagua mandhari ya video, rangi ya video, kubuni scene au maigizo yoyote yatakayotokea kwenye video nk….Kifupi sio kazi ndogo kama wengi wanavyofikiria.

Na katika hali hiyo kibongo bongo unakuta mwenye gari kazima simu hataki kuja tena, video queen nae kazingua, location wanalalamika muda umekwisha, vitu vyote hivi vinamlazimu director afanye maamuzi magumu ili msanii asipate hasara kwenye kazi yake. Mara nyingine msanii huyo huyo ndio manager ndio mshika fedha, ndiye dereva wa kwenda kuchukua watu.

Mimi kama Mtanzania nitaendelea kufanya kazi na mtu ambaye anahitaji msaada wangu na anapokwama nitamsaidia bila kujali kama ana budget kubwa au ndogo chamsingi tuelewane na tuheshimiane. Nilinde na mimi nitakulinda bila kujali wewe ni nani, na unatoka wapi.
Tatizo la Lugha
Kuna tatizo kubwa la lugha kitu ambacho kinafanya hii ishu ionekane kubwa wakati nikaishu kadogo sana. Mtu yoyote anaweza kufanya na video ikachezwa bila hata ya mbwembwe zozote. Inasikitisha kuona kwamba inabidi kulipa mamilioni ya fedha ili kuweza kupigwa kwenye TV hizo. Kuna kitu huelewi unaweza kuwapigia simu MTV Base kujua kama wamepokea kazi yako au hapana, contact hizi nimezipata baada ya kutafuta kwenye google tu Mtvbase contact kitu ambacho mtu yoyote anaweza fanya.

MTV Base CONTACT US
MTV Networks Africa (Pty) Ltd 
Physical address: No 1 Saxon Road, Hyde Park, Johannesburg, 2196
TEL: +27 11 4282900
TRACE SOUTH AFRICA
Valentine Gaudin – General Manager
TRACE South Africa
1st floor, The Design District
7 Keyes Avenue cnr, Tyrwhitt Avenue
Rosebank 2092
South Africa
Tel : +27 11 035 5500
southafrica@trace.tv
TRACE NIGERIA
Sam Onyemelukwe – Managing Director
1 Danny Estate, Makoko Road
Adekunle, YAba
Lagos, Nigeria
Tel : +234 (0) 1 842 – 5821
nigeria@trace.tv
Ushauri kwa wasanii na madirector


Kwa wasanii na madirector ushauri wangu wa bure ni kutembelea hizi site na kuelewa maelekezo na kuyafata, mtakubaliana nyie wenyewe sasa nani asimamie hiyo shughuli ya kupeleka video kwenye Tv hizo. Kila mtu awe huru kufanya kazi anapojisikia ili awe huru na kazi anayofanya, ila msiwe na nidhamu ya uoga ya kufikiria kwamba wewe kama msanii au director wa kitanzania huwezi kupeleka kazi kisa umeshot Tanzania au kwa mtu fulani.

Kama mtu anahitaji form za Trace, Channel, MTV Base na BET anaweza kunicheki kwenye email mtupah@yahoo.com ntakutumia, kama unahitaji maelekezo ntakuelekeza.

Msanii kama unaona ni ishu kubwa tafuta management, manager, record label wakusaidie.
Why record label????? Sio director?

Ikitokea deal kubwa watu wa Trace, Channel O, Mtv au BET wakianza kukutafuta wasianze kupitia kwa watu fulani fulani wakupigie wewe mwenye direct na team yako. Mimi siku zote naogopa lawama na kama kuna mtu au watu wataniona mbaya basi ni sawa tu ila hali ndio hii. Natanguliza shukrani kwa watanzania wote.

Regards,


Adam Juma.

Source:Bongo5
Previous Post Next Post