French Montana akanusha kuwa hayuko na Khloe Kardashian kwasababu ya umaarufu wake

Rapper wa ‘Don’t Panic’, French Montana amelazimika kutoa ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa kwenye mahojiano na jarida la Billboard kuwa anatumia umaarufu wa mpenzi wake Khloe Kardashian kwa faida.



Huenda wakati anatoa kauli hiyo alikuwa anamaana tofauti na ilivyotafsiriwa na watu mbalimbali waliomshambulia kwa kumtumia Khloe.

Montana ameiambia Access Hollywood Live kuwa comment yake ilitafsiriwa vibaya na hilo limemchukiza kwasababu anapodate na mtu huwa si kwa sababu ya umaarufu wake.“I was so mad about that, If I’m with somebody, I’m not with them for that reason.”



Aliendelea kuzungumzia uhusiano wake na Khloe,

“Ananisupport kwa kila kitu nachofanya. Na ikija katika career yake na mimi huwa siwazi, kama akinihitaji nifanye kitu nafanya”. Alisema

Hata hivyo Khloe hapo kabla naye alitweet kuwa hajali kauli aliyotoa Montana sababu yeye ndiye wa kwanza kuona mahojiano hayo, so watu wasidhani ameipokea kama wanavyodhani.
Previous Post Next Post