Diamond apewa shavu katika ngoma ya KCEE wa Naija, kufanya collabo na msanii mkubwa kutoka US!

Wasanii wa Nigeria wameendelea kumtafuta Diamond Platnumz kwaajili ya kumshirikisha kwenye nyimbo zao. Baada ya kushirikishwa na Waje na Dr Sid, msanii mwingine mkubwa anayetamba na nyimbo kama ‘Limpopo’ na ‘Pull Over’ KCEE ameomba kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya.



“Kuna nyimbo nimefanya na KCEE wa ‘Limpopo’ ni nyimbo yake by the way ambayo naenda kurekodi sasa hivi” Diamond alikiambia kipindi cha Hitlist cha Choice FM Alhamis iliyopita. “Nina project nyingi sana hadi naogopa kuzisema nyingine kwasababu sijaruhusiwa,” aliongeza.

Mshindi huyo wa tuzo 7 za KTMA 2014, aliongeza kuwa kabla mwaka huu haujaishia, mashabiki wake wategemee kupata zawadi ya wimbo aliomshirikisha msanii mkubwa wa Marekani. “Wategemee pia collabo nyingi sio kutoka Afrika, kutoka nje ya Afrika kabla ya mwaka haujaisha,” alisema Diamond japo alikataa kusema ni msanii gani.
Previous Post Next Post

Popular Items