Diamond adai dharau na mapozi ya waongozaji, vilimfanya aache kushoot video Tanzania

Pamoja na kutafuta video zenye kiwango cha juu zaidi, dharau na mapozi ni sababu kubwa zilizomfanya Diamond aache kushoot video zake kwa kutumia waongozaji wa video nchini.



Akiongea na Vanessa Mdee kwenye kipindi cha The Hitlist cha Choice FM jana, Diamond alidai kuwa alishasusa fedha nyingi kwa muongozaji wa video aliyemletea dharau wakati akidai haki yake.

“Sababu director unamlipa hela kwanza haheshimu kwamba wewe ni msanii anakuona kama unaenda kumuomba anaona kama unambembeleza,” alisema. “Hela umemlipa na atashoot siku atakayojisikia yeye kutokana na mood zake, haiwezekani hii ni biashara. Siwezi kukulipa milioni 40 halafu ukanipangia masharti unayotaka wewe wakati nakulipa na nimerekodi nyimbo yangu mimi najua nataka nifanye kitu gani. Mtu utamlipa atataka akuletee pozi, uamke saa 12 asubuhi yeye afike saa nne,” aliongeza.

“Kule [nje] unalipa unaona kabisa anaiheshimu kazi yako. Mimi nimeshasusa hela sikushoot video ya ‘Lala Salama’, sikushoot ‘Nimpende Nani’ video sababu hela nilikuwa nimeshatoa lakini video nimezungushwa kwa zaidi ya miezi mitatu so mtu utaweza kuvumilia usubiri? Ndo hapo mimi nikaacha kushoot video Tanzania. Mwanzoni sikuwa na fikira kwamba Tanzania hatuna quality nzuri, nilikuwa naona kwamba ‘ahh’ tunaweza;, lakini baada ya kuona nilishalipa hela nab ado nanyanyasika kwa hela yangu mimi mwenyewe, nikaona ‘you know what ngoja nitafute sehemu nyingine.”

Previous Post Next Post