Baada ya Gwajima kununua Helikopta, Askofu Kakobe ameyasema haya.

Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook twitte na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.



Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’

‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe




Kuhusu Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu, mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana’
Previous Post Next Post