Uholanzi yashika nafasi ya 3 katika Kombe la Dunia 2014

TIMU ya Uholanzi imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil.

Mabao ya Robin van Persie dakika ya 3, Daley Blind dakika ya17 na Georginio Wijnaldum dakika ya 90 yalitosha kupeleka vilio tena kwa mashabiki wa Brazil walioamua kuwazomea wachezaji na kocha wa timu yao Felipe Scolari.

Kwa kipigo hicho, Brazil wamefungwa mabao 10 katika mechi mbili ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani na hii ya mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi.

Wachezaji wa Uholanzi wakipozi na medali zako baada ya kushika nafasi ya tatu Kombe la Dunia 2014.

 Robin van Persie akiifungia Uholanzi bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya tatu ya mchezo
Robin van Persie akishangilia na mwenzake Dirk Kuyt (juu) baada ya kufunga bao la kwanza kwa Uholanzi.

 Beki wa Uholanzi, Daley Blind (kushoto) akitupia kambani bao la pili katika dakika ya 17.

Wachezaji wa Brazil waliokuwa benchi pamoja na Neymar wakiwa na majonzi ya kipigo kingine cha 3-0.
Kipa wa Brazil, Julio Cecar alivyonaswa baada ya bao la 3 lililofungwa na kiungo Georginio Wijnaldum dakika ya 90.


Previous Post Next Post