Timaya wa Nigeria asema alitumia zaidi ya milioni 200 kukamilisha collabo na Sean Paul

Msanii wa Nigeria, Timaya ameeleza kuwa alitumia zaidi ya N20m (zaidi ya milioni 200 za Tanzania) kukamilisha collabo aliyofanya na Sean Paul katika remix ya wimbo wake ‘Bum Bum’.

Msanii huyo amesema kiasi hicho cha pesa kilitumika katika kutengeneza audi na video ya wimbo huo.


Pamoja na kutumia kiasi hicho cha pesa, ilimchukua miezi 6 ya mipango hadi kukamilisha zoezi zima.

“Nilitumia zaidi ya N20m katika wimbo huo na video. Ilinicost kiasi hicho kumleta Sean Paul na watu wake kutoka Jamaica, sitanii.” Timaya aliiambia Toolz.


Previous Post Next Post