Picha: Video ya Prokoto yaanza kushutiwa Dar na Director kutoka kenya, Diamond Platnumz , Victoria Kimani na Ommy Dimpoz

Mkenya  Victoria Kimani kutoka katika lebo Choclate City ya Nigeria, alikuwepo nchini kwa kwaajili ya utengenezwaji wa video ya single yake ‘Prokoto’, aliyowashirikisha Diamond na Ommy Dimpoz ambayo audio tayari ilishatoka.



Video hiyo ilishutiwa jana (July 11) jijini Dar es salaam na kuongozwa na director Kevin Bosco wa Kenya aliyeongoza video ya AY ‘Asante’.



 Diamond aliyewasili nchini Juzi uziku (July 10) akitokea Marekani, pamoja na Ommy Dimpoz ambao wote wameshirikishwa kwenye wimbo huo wameshiriki pia katika video.



Kupitia ukurasa wa Instagram wa WCB_Wasafi ya Diamond walipost picha ya Dimpoz, Diamond na Victoria wakiwa kwenye moja ya locations.

Previous Post Next Post