Picha: Neymar aendelea kuuguza majeraha ya kombe la dunia akiwa na mpenzi wake Bruna Marquezine

Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar ameendelea kupata nafuu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa kombe la dunia na hivyo kuamua kwenda vekesheni kidogo na mpenzi wake Bruna Marquezine nchini Hispania.

Neymar na Bruna Marquezine

Wawili hao wameonekana wakitumia muda wa pamoja kupunga upeo kwenye fukwe za Formantera. Mchezaji huyo bado amefungwa na kitu cha kuushikiliza mgongo wake. Neymar alishindwa kuendelea na mechi za kombe la dunia baada ya kujeruhiwa mgongo wake kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia. Tazama picha zaidi za likizo yao.







Previous Post Next Post

Popular Items