Obama: Ndege ya Malaysia imetunguliwa na waasi wa Ukraine wanasaidiwa na Urusi

Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ana ushahidi unaoonesha kuwa ndege ya Malaysia, Flight MH17 iliyoluwa kisafiri kutoka Amstaderm kwenda Kuala Lumpur ilitunguliwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi.


Amesema kitendo hicho kinatia hasira kwa kuzingatia maisha ya watu wasio na hatia 298 waliopoteza maisha katika tukio hilo na kwamba ushahidi huo unaonesha kuwa bomu hilo lilirushwa na kutoka eneo linalodhibitiwa na waasi hao ambao hupokea misaada ya makombora kutoka Urusi.



Obama ametaka mapigano yanayoendelea Ukraine kusitishwa ili kutoa fursa ya shirika huru la kimataifa kufanya uchunguzi.
Previous Post Next Post