Madaktari wagundua mwanaume yuko kwenye 'hedhi'

Dunia ina mambo na tembea ujionee, wiki hii tuliandika habari kutoka China iliyohusu kijana aliyeng’olewa meno 132, lakini pia kuna habari nyingine kutoka nchini humo ambayo imewaacha wengi midogo wazi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Shagalist, mwanaume aliyetajwa kwa jina la Mr. Chen, mwanandoa mwenye umri wa miaka 44 na mkaazi wa Zhejiang, China amegundulika kuwa alikuwa katika siku zake kama inavyokuwa kwa wanawake kwa mzunguko wa hedhi(period) baada ya kufika hospitali akilalamika sana kuwa na maumivu ya tumbo.



Taarifa zilizotolewa na madaktari wa hospitali ya Yongkang zinaeleza kuwa mwanaume huyo alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa alikuwa na mfumo wa uzazi wa mbegu za mwanamke ingawa alikuwa na uume.

Ingawa mwanamme huyo aliwaeleza madatari kuwa amekuwa akishiriki na mkewe tendo la ndoa kwa miaka kumi ya ndoa yao bila tatizo, madaktari hao waligundua kuwa alikuwa anatoa mkojo wenye damu ambao uliwasababisha wafanye uchunguzi wa kina na kugundua hali hiyo.

Msemaji wa hospitali hiyo alieleza kuwa vipimo vya ACT Scan vilionesha wazi kuwa alikuwa na uterus na ovaries (mayai ya uzazi), na kwamba madaktari walieleza kuwa alikuwa amechelewa kupata matibabu kwa tatizo lake hilo lisilo la kawaida.

Mr. Chen mwenyewe alieleza kuwa alikuwa anasikia dalili ya vitu vingi visivyo vya kawadia hata katika maumbile yake, na kibaya zaidi ni pale alipoanza kuona anatoa damu badala ya haja ndogo.
Previous Post Next Post

Popular Items