Maajabu: Madaktari wamng'oa kijana meno 232, walitumia Nyundo na tindu

Maajabu hayaishi katika dunia hii, wakati ambapo kinywa cha binadamu mtu mzima kinakadiriwa kuwa na meno 32, Ashik Gavai, kijana mwenye umri wa miaka 17 ameng’olewa meno 232.

Kwa mujibu wa BBC, madaktari nchini India wametumia saa saba kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana huyo aliyekuwa na maumivu kinywani kwa muda mrefu.


Dr Sunandrea Dhiware, mkuu wa kitengo cha tiba ya meno kaitika hospitali ya JJ iliyoko Mumbai, India ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinnywani mwa kijana huyo aliyefikishwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya na kulalamika kuwa ana maumivu makali.



Meno yaliyong'olewa

Madaktari hao wameeleza kuwa katika upasuaji huo uliohusisha jopo la madaktari wane walilazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa men ohayo na kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.

Dr Dhiware ameeleza kuwa kwa uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari hajawahi kukutana na tukio kama hilo na kwamba hata katika vitabu alivyosoma alielezwa kuwa katika historia yaliwahi kung’olewa meno 37 katika taya la juu lakini hii imekuwa meno 232 tena katika taya la chini.
Previous Post Next Post

Popular Items