DNA sasa abadli jina, ajiita 'Bwana DNA'

Rapa DNA wa nchini Kenya ambaye awali alikuwa anafahamika kwa jina DNA hivi sasa anajiandaa kuliacha jina hilo na kujiita ‘Bwana DNA’.


Rapa huyo ambaye hivi sasa anafanya muziki wa injili ni takriban mwezi mmoja tokea aachane na lebo ya Grandpa kutokana na kukosa shows na dili mbalimbali akiwa ndani ya lebo hiyo.
Hivi sasa 'Bwana DNA' kama ambavyo amejibatiza jina hilo amesisitiza kuwa ukiwa una google kutafuta jina la DNA unaletewa maana nyingi ambazo hazimpendezi, hivyo ameamua kuongezea neno 'Bwana' ili liwe la kipekee zaidi.

Previous Post Next Post