Diamond kutoa video nyingine ya ‘Mdogo Mdogo’, itaonesha watu wakicheza zaidi

Diamond Platnumz anataka kuwapa mashabiki wake zawadi nyingine ya video ya Mdogo Mdogo. Kupitia shindano la kucheza wimbo huo alilolianzisha na kuahidi kumtunza shilingi milioni moja mshindi, staa huyo amesema atatoa video itakayoonesha namna ya kucheza style ya wimbo wake akiwa na washindi hao.


Kupitia Instagram, Diamond ameandika:

Nafikiri sasa ni wakati Muafaka, Mi shida yangu ni Moja tu, nahitaji nipate style maalum ya kucheza #Mdogomdogo .. iwe kutoka kwa Kundi au mtu yoyote kutoka nyumbani… ukiwa unaamini unaweza kutoa style na ikatumika kama Mdogomdogo Dance tafadhari ntumie kuanzia sasa Kwenye namba hii +255652427989 au ipost kwenye Instagram yako kisha hash tag neno #MdogoMdogoDance nami nitairepost hapa (instagram)… Mwendo ni ule ule tu, Kikundi au mtu atakaekuwa na Likes nyingi ndio tutaichukua Style yake na kuwa official dance style ya #MdogoMdogo .. Pia atapata Shilingi Milioni Moja Cash! na Kuwepo kwenye video mpyaaa ya Kucheza tu, iitwayo #Mdogomdogo_Instructional_Video pamoja na Team Nziiima ya Wasafi.



Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA