Audio: Madaktari washikiliwa kwa tuhuma za kutupa viungo vya miili ya binadamu Dar


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wanane wakiwemo madaktari wa chuo cha udaktari cha IMTU kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la viungo vya binadamu vilivyokutwa katika bonde la Mbweni mpiji eneo la Bunju.



Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kamishina wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Sulemani kova amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa miili hiyo imethibitika kutoka katika chuo cha udaktari cha IMTU

Aidha kamishina kova amesema kuwa katika tukio hilo walikuta mifuko 85 ambayo ilikuwa imebeba viungo vya binadamu vilivyokaushwa vikiwemo vichwa, miguu, mikono, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali.




Amesema kuwa jeshi la polisi limeunda jopo la watu 7 likiongozwa na mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar es salaam kamanda Jaffary Mohamed hivyo amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao huku uchunguzi wa kina ukiendelea

Kamanda Kova amesema uchunguzi huo utabaini endapo kuna uhalifu au uzembe uliofanyika na hatua za kisheria zitachukuliwa dhi
di ya watakaobainika kuhusika.

Lakini pia amewataka watanzania kutolihusisha tukio hilo na masuala ya kishirikina au upotevu wa watu hadi hapo jopo litakapotoa taarifa rasmi baada ya uchunguzi kukamilika.

Msikilize hapa:




Source:TimesFm
Previous Post Next Post