Ahadi ya Rais Kikwete yatimia, baada ya Mtangazaji wa E! Entetainment TV ya Marekani kuthibitisha kuja Tanzania

Ile ahadi aliyoitoa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete hivi karibuni ya kuwaleta baadhi ya watu muhimu wa sanaa duniani kwaajili ya kuzungumza na wasanii wa Tanzania inaelekea kutimia.




Miongoni mwa majina aliyoyataja Rais kuwa watakuja kuzungumza na wasanii wa Tanzania ni pamoja na mtangazaji wa E! Entetainment TV ya Marekani Terrence J, ambaye jana (July 9) amethibitisha ujio wake wa Tanzania.

Kupitia Instagram Terrence J aliandika: “Headed to Tanzania to give back, learn new cultures, and marvel at Gods work. I’ve never been to Africa and I’m overwhelmed with joy. I look forward to coming back a better man. Love y’all, see you soon. God bless, T”
Previous Post Next Post

Popular Items