Video: Huyu ndiye muhalifu Handsomeboy , wasichana duniani wavutiwa naye

Kweli Dunia inavioja, mhalifu kutoka Marekani amefanikiwa kuziteka roho za wasichana wengi duniani kote baada ya polisi kupost picha (mugshot) kwenye Facebook na kuvutia zaidi ya likes 40,000.


Jeremy Meeks ametokea kupendwa na wasichana wengi baada ya polisi Stockton Police Department kupost picha yake kuelezea kukamatwa kwake. Meeks, alikamatwa na silaha kutokana na msako wa polisi kubaini magenge ya uhalifu kwenye mji huo uliopo kaskazini Californian.
Hata hivyo polisi hao hawakupata mrejesho walioutegemea kwakuwa maelfu ya wanawake walionesha kuvutiwa naye.



Tinish Anderson aliandika: “Model material. His jawline. Lol i ain’t thirsty but whew” huku Anita Gibson akiandika “Smoking hot!”.
Princess Jade aliandika: “Lock me In his cell yummy” huku wengine wakitania kutaka kumtolea dhamana.
Previous Post Next Post