Rais Kikwete amkutanisha Diamond na Rais wa zamani wa Def Jam na meneja wa Trey Songz, Kevin Liles

Siku chache zilizopita staa wa bongofleva, Diamond Platnumz alikutana uso kwa uso na Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani muheshimiwa Raisi Kikwete Huko New York Mareani, sababu ya Raisi kukutana mkali huyo wa bongo fleva ni katika kuendeleza harakati zake na kuthamini kazi za wasanii wa Tanzani ili kuwapa support waweze kufikia malengo yao na kukuza muziki wa Tanzania kimataifa

Ambapo baada ya staa huyo kufanya Kolabo na manii wa Nigeria Davido na kumzidishia umaarufu mkubwa, sasa anatarajiwa kufanya kolabo na msanii wa Marekani Trey Songz. Kama Diamond atafanikiwa kufanya kolabo na msanii huyo basi Raisi Kikwete atakuwa ndie ameshiriki na kutoa mchango mkubwa katika kulikamilisha hilo




Ukubwa wa muziki wa Diamond umefanya Rais Jakaya Kikwete akutane na aliyekuwa rais wa Def Jam Recordings na makamu mkuu wa rais wa The Island Def Jam Music Group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004, Kevin Liles ambaye kwa sasa ni meneja wa Trey Songz, Big Sean na Estelle.

Ni ngumu kufahamu nini walichokuwa wakizungumza lakini kuna ishara kubwa kuwa mazungumzo hayo yatazalisha kitu kikubwa ambacho kama sio collabo ya Diamond na msanii mkubwa wa Marekani (wakiwemo anaowasimamia Liles) basi ni connection itakayompeleka hitmaker huyo wa ‘Number One’ level nyingine kubwa.

“Wapi utapata Rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao unatafutwa karibu na kila mtu duniani..akautumia kukusaidia kukukutanisha na kukuconnect na mdau mkubwa duniani katikaa tasnia uliyopo, ili kuhakikisha tu Unafikia Malengo na Ndoto ya kazi zako…. Dah! Asante sana Mh Rais, Mwenyez Mungu akuzidishie na kukusmamia katika uongozi wako na siku zote za Maisha yako,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

Maelezo hayo yanaonesha kuwa Rais Kikwete amehusika kwa kiasi kikubwa katika kumkutanisha na Kevin Liles, mtu anayeheshimiwa mno kwenye muziki wa Marekani. Diamond amekutanishwa na mtu sahihi Marekani, mtu ambaye anazijua ramani zote za muziki wa nchi hiyo na mtu ambaye ana uwezo wa kumuunganisha na label yoyote kubwa duniani ambayo kwa ushawishi alioupata Diamond barani Africa na nomination ya BET Awards anastahili.
Previous Post Next Post