Professor Jay na AY wamkabidhi Rais Kikwete maoni ya wakulima na changamoto zao

Balozi wa taasisi ya kilimo isiyo ya kiserekali (Ansaf) Professor Jay, pamoja na AY ambae ni balozi wa ( OneCampaign ) taasisi ya kilimo isiyo ya kiserekali, wamemkabidhi Rais Kikwete taarifa ya maoni kutoka kwa wakulima wa Tanzania, katika mkutano wa maswala ya kilimo uliyofanyika hotel ya DoubleTree jijini Dar hapo jana.


Professor Jay na Mrisho Mpoto wakiwa katika shughuli za kuhamasisha kilimo.

Professor ameiambia bongo5 kuwa akiwa na mabalozi wenzake wa Ansaf, Mrisho Mpoto pamoja Masoud Kipanya, kupitia kampeni ya ‘DoAgric’ waliweza kukusanya maoni mbalimbali ya wakulima na kumkabidhi Rais Kikwete ili serekali iyafanyie kazi.

“Sisi kama mabalozi wa Ansaf tulikabidhi saini za wakulima, kuna kituo kimoja cha radio kinaitwa Farmers Radio, kilifanya research na wakawatembea wakulima kadha sehemu tofauti tofauti na kuangalia wakulima wanamatatizo gani na nini kifanyike ili kuwasaidia wakulima wa Tanzania na Afrika nzima kwa umoja , so mimi kama balozi jana nilichokifanya nilikabidhi signature za wakulima wa Tanzania zaidi ya milioni 2 , kwa mweshimiwa Rais Kikwete ambao wengi waliweka matatizo yao ,wameweka hoja zao ambazo zinawakabili ili kwa upande wa serekali waweze kuzifanyia kazi na pia kumwagiza Rais wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania haende kuliongea hili katika mkutano mkuu wa Afrika , 2013 walikuwa wanadhamira ya kuwekeza kwenye kilimo, na mwaka huu 2014 umechaguliwa kama mwaka wa kilimo kwaiyo Rais atakuwa huko Maputo Msumbiji baadae ,wanamkutano wao , pia tumemwagiza Rais akaliongelee hili swala la changamoto za wakulima wadogo wa Tanzania na Afrika nzima’’Alisema Professor Jay.


Balozi wa OneCampaign Tanzania, AY akiwakilisha maoni kwa Rais Kikwete
Kwa upande wa AY ambae ni balozi wa One Campaign, amesema kuwa yeye kama balozi kupitia barua yake ameishauri serekali ya Tanzania kuungana na nchi mbalimbali za Afrika kutatua changamoto za wakulima.

“Cha msingi lazima tufanye juu chini kilimo kiwe juu, kwaiyo Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazichangiti asilimia kumi kwenye kila bajeti ya mwaka kuwekeza kwenye kilimo, kwaiyo ule ujumbe unatakiwa umshawishi Rais kuanzia mwaka huu wawe wanatenga asilimia kumi au zaidi ya asilimia kumi kwajili ya kuwezesha sekta ya kilimo, kingine ni kwamba ku motivate vijana kwenda kwenye kilimo kwa sababu kilimo kinakaa kama nicha watu masikini au kama cha wazee, wakati vijana tukiweza kujikita kwenye kilimo mpaka kufika 2030 tutakuwa tupo mbali sana, kwaiyo ujumbe wangu nilimkabidhi Rais akaupokea, na akatoa speech yake, akasema ujumbe umefika, Pia akasema kabla ata hajaenda, kwa sababu anamkutano huko Malawi na Equatorial Guinea juni 25 mpaka juni 27 ,atapeleka ujumbe kwa wahusika na litashughulikiwa” Alisema AY
Previous Post Next Post