Picha/Video : Majambazi waua sista na kumkata kidole dereva kwa risasi Dar - River side 'Ubungo'

Hali ya hewa imechafuka kwa wakazi wa eneo la Ubungo-Darajani karibu na River Side baada ya majambazi kumuua Sista wa Parokia ya Makoka-Mwisho aliyefahamika kwa jina moja la Kapuli na kisha kumjeruhi dereva wa gari na kutokomea na mkoba wa marehemu kusikojulikana.

Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.


Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu jana mchana wakati sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa lengo la kununua mahitaji muhimu.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.



Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi dereva huyo kidoleni.

Gari alilokuja nalo marehemu Sista Kapuli.

Gari alilokuja nalo marehemu Sista Kapuli.



Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.

Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio.

.Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.


Source:Gpl
Previous Post Next Post