Ommy dimpoz amedharau mashabiki au karudisha upendo?

Jumapili ya Juni 1, 2014 ommy dimpoz alikuwa miongoni mwa wasanii waliohudhuria shoo kubwa ya uzinduzi wa kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam uliofanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga.

Wakati akipanda jukwaani , mashabiki kwa mamia , hawakuwa wamechangamka kama alivyotegemea na ili kuwaamsha, alivua kofia yake na kuwatupia .Baada ya hapo akawatupia pia miwani na baada ya kutupa vitu hivyo alitoa shilingi elfu hamsini na kuwarushia.



Ommy Dimpoz akawageukia mashabiki nakuwaambia maneno haya “Sisi wasanii tunapata fedha nyingi kutoka kwenu nyinyi mashabiki wetu, kuonyesha kuwajali , naomba niwarudishie.” Hiyo tisa , kumi, Dimpoz alizama tena mfukoni na kuibuka na kiasi cha kama laki mbili hivi na kuwarushia tena watu waliojazana mbele yake !




Kitendo alichofanya Ommy Dimpoz kimezua mijadala mingi hasa kwenye baadhi ya mitandao ikimponda ommy dimpoz kwa kuchezea pesa kwa kudai anarudisha kwa mashabiki badala ya kurudisha kwa njia sahihi kama kurahisisha huduma za maji na mengineyo. Kwa mtazamo wangu kitendo alichofanya ommy dimpoz ni sahihi kwani pesa alizotupia mashabiki zinaweza kua sawa na thamani ya kofia au miwani aliyowatupia na hata kama si sawa basi kuna tofauti gani watu wakitupiwa kofia au miwani ya dimpoz na kuanza kugombania na wanapotupiwa pesa ? Tena pesa inakua ni vizuri zaidi sababu mashabiki wengi watapata pesa hizo ukilinganisha na watu wawili watakaoondoka na kofia au miwani.






Katika moja la onyesho nchini Marekani ambapo mwanamuziki Juicy J alikua akiimba pamoja na miley cyrus, juicy aliweza kurusha pesa zenye thamani ya dola 5000 sawa na shillingi millioni nane za kitanzania na kussema haya baada ya hapo. Ni Bora kwa shabiki aliyekaa mbele ya stage kumpa support Ommy Dimpoz apate pesa ya kunywea chai kesho au ommy dimpoz aendelee kuiweka pesa hiyo mfukoni ?
We unaonaje, Ommy kutupia pesa mashabiki wake unadhani ni sahihi au sio sahihi?
Previous Post Next Post