Kocha wa Hispania akubali lawama baada ya kutolewa mapema kwenye fainali za kombe la dunia

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque amesema hana njia ya mkato ya kusema samahani kwa mashabiki wa soka wa nchi hiyo kufuatia kikosi chake kushindwa kuonyesha uwezo wa kutetea ubingwa wa kombe la dunia.

Vicente del Bosque amesema kikubwa anachokiona mbele yake ni kukubaliana na hali halisi iliyoonekana tangu waliponza akampeni ya kutetea ubingwa wao juma lililopita, kwa kufungwa mabao matano na Uholanzi na kisha kupoteza mbele ya timu ya taifa ya Chile.



Amesema kikosi chake hakikucheza vizuri tangu mwanzoni mwa fainali za mwaka huu, na hali hiyo imekuwa dhambi kubwa sana kwao na kujikuta wakiondolewa mapema tofauti na ilivyokuwa inafikiriwa.

"Hatuna sababu za kujetea, zaidi ya kukubaliana na hali iliyoonekana uwanjani tangu kwenye mchezo wa kwanza," amesema del Bosque.

"Kikosi changu kimecheza chini ya kiwango tangu dakika ya kwanza ya mchezo dhidi ya Chile, na matokeo yake tumeambulia adhabu ya kufungwa mabao mawili kwa sifuri yanayotutupa nje ya michuano hii’’ Ameongeza kocha huyo.

Kwa upande wake mlinda mlango pamoja na nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, Iker Casillas amesema ni vigumu kuamini kilichotokea uwanjani hapo jana, lakini hawana budi kukubaliana na hali hiyo ambayo ulimwengu mzima imeiona.

Previous Post Next Post

Popular Items