Ray C alazwa Mwananyamala kwa ugonjwa wa Dengue

Msanii wa muziki, Rehema Chalamila aka Ray C amelazwa katika hospitali ya Mwananyala wodi namba tano kutokana na ugonjwa wa Dengue

Ray C akiwa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala

Akizungumza na gazeti la Mwananchi ,Daktari ambae alikataa kutajwa jina lake,alithibitisha kulazwa kwa Ray C kutokana na ugonjwa huo jana. “Tumethibitisha kwamba Ray C ana dalili zote za dengue, lakini kimaadili siruhusiwi kutoa taarifa za mgonjwa,” alisema daktari huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake. Hata hivyo,kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi limethibitisha kumwona mwanamuziki huyo hospitalini hapo akiwa katika usingizi mzito na madaktari walisema hakuwa katika hali mbaya bali alikuwa amelala kwa sababu ya uchovu wa dawa.

Mbali na Ray C, pia madaktari watatu na muuguzi mmoja wameripotiwa kuugua ugonjwa huo.

Tayari mamlaka zimetoa tahadhari kwa wananchi kuwataka wachukue hatua za haraka kuzuia maambukizi ya homa hiyo inayosababishwa na mbu anayejulikana kitaalamu kama aedes egyptiae. Hadi sasa wagonjwa zaidi ya 100 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke na baadhi wakiripotiwa kupoteza maisha.

Daktari kiongozi wa hospitali hiyo ambaye pia ni mtaalamu wa ugonjwa huo, Dk Mrisho Rupinda alisema kuwa kuna taarifa za wagonjwa wa dengue walioripotiwa katika maeneo yote ya Dar es Salaam.

“Katika kipindi cha wiki moja iliyopita tayari madaktari wawili kwenye hospitali hii wamebainika kuugua ugonjwa huo, tunahisi walipata maambukizi kwenye maeneo ya humuhumu ndani hospitali,” alisema Dk Rupinda.
Source:Mwananchi
Previous Post Next Post