Picha/Video: Diamond achukua tuzo saba za kill, Fid Q na Weusi watamba kwenye hip hop

Diamond Platnumz amethibitisha kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.



Msanii mwingine aliyeshangaliwa zaidi katika usiku wa tuzo hizo ni Fid Q aliyenyakua tuzo mbili ambazo ni Msanii Bora wa Hip Hop na Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop.

Isha Ramadhan akipokea tuzo


Wasanii wa Kenya, Amani na Wyre wakimkabidhi tuzo Luiza Mbutu






Wema akimkumbatia Diamond


Tazama video hapa Diamond Platnumz akiongea Baada ya Kupkea Tuzo.



Vanessa Mdee akimbusu Lulu baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa R&B





Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akimkabidhi Fid Q tuzo

Nalo kundi la Weusi limeibuka na tuzo mbili, Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako) na Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya.



Bonnie Luv akimkabidhi tuzo Fid Q



Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi tuzo Diamond, kushoto ni producer wa My Number One, Sheddy Clever

Ommy Dimpoz akiongea kwa niaba ya Diamond Platnumz

Muimbaji huyo aliyekuwa ameambatana na mchumba wake Wema Sepetu amechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa afro pop na video bora ya mwaka kwa wimbo wake ‘My Number On’e pamoja na Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki na Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya.

credit:Bongo5
Previous Post Next Post