Mambo Matano (5) ya kujiuliza Kuhusu Mahusiano Katika Mwaka 2014

Kwanza kabisa kama unaisoma post hii, hii inamaanisha Mungu amekuweka hai na unaendelea na mambo yako katika mwaka huu wa 2014. Hongera sana kwa kufika na natumai utakuwa ni mwanzo mzuri wa mengi yenye manufaa katika maisha yako;


Leo natamani sana tuzungumze juu ya Mahusiano kidogo. Huu sio wakati wa kupotezeana muda katika mahusiano, huu sio wakati wa kuplay around na feeling za watu. mimi ninayo maswali kadhaa natamani ujiulize ukiwa unaendelea na mwaka huu wa 2014
  1. Je huyo mpenzi uliye nae kwa mwaka huu hadi unaisha amekuletea faida/ positive effects kwa kiasi gani. umenufaika vipi kuwa nae, amekushaur mazur kwa kiasi gani, anakusaidia kuyafikia malengo katika maisha kwa kiasi gani, huwa mnakaa na kujadili mambo ya msingi mara ngapi. AU ndo huwa mkikutana ni mnawaza tu leo bata wanaliwa wapi na mengineyo?
  2. Ni kweli kabisa unampenda kutoka moyoni na unadhani ni yeye unamuhitaji katika maisha? Au bado umekusanya lundo la wapenzi na haujui hasa ni nani unaemuhitaji. Mimi nadhani ni wakati wa kuacha kujitesa hata wewe kwa kudanganya sana watu kwani idadi ya wapenzi ikishazidi mmoja inamaana unajipa kazi ya kuugawa moyo wako katika vipande, kujitesa kudanganya kusiko kwa lazima, kujiweka kwenye mtandao ambao ni rahisi sana kuyapoteza maisha yako kwa magonjwa ya zinaa na UKIMWI jipende jithamini na yapende maisha.
  3. Sijui mlikutana vipi na mkaanza vipi mahusiano yenu. Lakini ni wakati wa kuangalia zaidi ya kila mtu aonavyo. unahitaji wa kuzugia, wa kupoteza nae mda, wa kufanya nae show off(maonesho) kwa jinsi alivyo hand some au beutful na ameumbika sn. hey zinduka uzuri hauliwi ndugu yangu. You need a lifemate mtu ambaye kwako atakuwa msaada na wewe utakuwa msaada. Unahitaji mwanaume wa aina gani, mwenye viwango gani, mwenye sifa zipi, hey wewe ndie unaemuhitaji anza kuwa na kanuni na viwango hivyo then fanya maamuzi ya makusudi. same to you mkaka unahitaji mwanamke wa aina gani na wa viwango gani unaweza kumpata ukiamua.
  4. Mmekaa kwenye mahusiano kwa mda gani. Tangu muwe kwenye mahusiano mpk leo mmechukua hatua gani ya msingi au miaka yote mpogo hivo hivo. ni wakati wa kuchukua hatua zingine zaidi. kama hamna mpango wa kuishi pamoja msipotezeane mda hebu kila mmoja aendelee na mambo yake ya msingi. Msizibiane nafasi ya kukutana na watu wenye malengo mazuri na nyie. Sio kesi wala dhambi kuachana endapo hamuioni future kati yenu. Fanyeni maamuzi sasa maana hakuna wakati mwingine.
  5. Upo nae kwasababu unamuonea huruma, kwasababu unajiuliza utaanzaje kumuacha, mmeshakaa mda mrefu sana, upo nae kwasababu ndugu zake karibu wote wanakufahamu na wewe umeshamtambulisha kwa ndugu zako wooote, upo nae kwasababu ndie anaekusaidia shida zako za hapa na pale za kifedha uko nae kwasabau tu hauna mtu mwingine? Au uko nae kwasababu amekulazimisha sana umkubali. kama sababu ni hizo na zinazofanana na hizo unafanya jambo la ajabu sana. Muache sasahivi maana unatengeneza na kuchimba kaburi utakalozikwa mwenyewe. Upendo wa dhati kutoka moyoni na kuridhika kuwa nae iwe sababu ya kuendelea kuwa nae na si vinginevyo.
MAPENZI YAPO MOYONI LAKINI PIA NI MUHIMU KUKUMBUKA HEBU ACHA AKILI IKUONGOZE KUFANYA MAAMUZI YA MOYO INAPOFIKIA KWENYE KUPENDA. SI KILA PAHALA NI PAKUPENDA OTHERWISE ITAKUCOST SANA. Akili kichwani mwako walioshtuka kwanz awalishafanya maamuzi sahihi mapema sana hata kama yalionekana kuwa mabaya kwa wengine. Ni bora umuambie ukweli mtu utakaomuumiza leo na atapona mapema na kukushukuru, kuliko umwambie uongo utakao muumiza hapo baadae na milele yote atakulaumu. NAWATAKIA MWAKA WENYE MAFANIKIO NA UPENDO MWAKA 2014
Previous Post Next Post

Popular Items