Cpwaa awasainisha Wadananda kwenye label yake ya Brainstormusic

Kundi la muziki wa kizazi kipya lijulikanalo kama “Wadananda” limebahatika kuingia mkataba na record label mpya nchini Tanzania ya “Brainstormusic”. Kampuni hiyo inayomsimamia msanii maarufu wa kizazi kipya ” CPwaa” imeamua kujitanua na kuanza rasmi kusimamia kazi na wasanii wa muziki,filamu,Michezo, Michoro,Vinyago,Upigaji picha pamoja na fashion.



Wadananda linalotengenezwa na vijana wawili “Kea Ahmedi kidato”(Customer Care) na “Natali Ali Katolila” (Pengo) wameingia mkataba huo na Brainstormusic mwezi wa pili mwaka huu na tayari hivi sasa wameshapikwa vizuri na wanategemea kuachia single ya mpya chini ya usamimizi wa label hiyo mwezi ujao. Wadananda waimeingia mkataba wa kurekodi album ya muziki, TV Shows, filamu na Management kupitia “Brainstormusic”. Mpala sasa wameshakamilisha photoshoots,nyimbo yao mpya, na taratibu za kushoot video ndio zinaendelea.
Wadananda watakua wasanii wa pili baada ya CPwaa kuingia mkataba na label hiyo ambayo imedhamiria kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya burudani. Wasanii wengine ambao wapo kwenye hatua za mwisho za kupitishwa na label hiyo ni chipukizi wawili ” Nurdin” na “Feisal”. Tayari kampuni hiyo imeshaini kikundi kimoja cha ngoma za asili na kwa sasa hivi bado wanapitia maombi mengi ya wasanii wa Hip Hop na Bongo flava.
Previous Post Next Post