Audio: Hizi ndizo sababu za Nikki wa Pili kufanya wimbo wake mpya wa 'Staki Kazi'

Wakati ambapo vijana wengi wakihangaika kutafuta kazi huku wengi wao wakiishia mtaani baada ya kumaliza kiwango fulani cha elimu, mshindi wa tuzo za KTMA Nikki wa Pili yeye amejipanga kuachia wimbo mpya May 13, akieleza umma kuwa hataki kazi.



Akiongea katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm na Omary Tambwe aka Lil Ommy, Nikki wa Pili ameuelezea wimbo wake na sababu zilimpelekea yeye kusema hataki kazi.

“Staki kazi simply kwa sababu kwanza ajira zenyewe ziko chake. Kwa hiyo mimi naona kwa nini vijana wengi wanaumiza kichwa kutafuta ajira ambazo ziko chache. Soko la ajira ni finyu, soko linachukua kama watu 50,000 mpaka 100,000 kwa mwaka. Lakini kwa mwaka watu wanaingia kama 600,000 kwenye soko la ajira.” Amesema Nikki wa Pili.

“Watoto wengi wanamaliza sekondari, chuo na wao wenyewe hawakujiandaa na ukosefu wa ajira. Mfumo haujawaandaa na wao wenyewe hawajajiandaa. Kwa hiyo Staki Kazi imekuja kushitua mentality yao kwamba…mtu anategemea okay Nikki wa Pili amesoma mpaka Masters na mtaani kwetu sisi ukiongelea ajira unaongelea kusoma. Watu wanasema ‘soma upate kazi’. Sasa mimi nimesema mimi nimeenda shule lakini Staki Kazi! Then watu watasema What! Na mimi nafikiria ni role ya mtu aliyeenda shule kutengeneza ajira kwa watu wa nyuma yake.”

Nikki amesema kuwa yeye anataka kuwa mtu ambaye atatengeneza ajira kwa watu wengi na sio kuajiriwa tu.

“Unajua kama mimi nitafanya kazi halafu sitasaidia watu wawili watatu itakuwa haina maana.”

Staki Kazi ni wimbo wake mpya ambao umetayarishwa na Nahreel na anauachia rasmi leo (May 13) na amewashirikisha G- Nako na Ben Pol..

Msikilize hapa akiongea



Credit:Timesfm
Previous Post Next Post