Audio: Fid Q Anastahili kuchukua tuzo, muda wake umefika ndio maana akachukua " Suma G "

Usiku wa May 4, ulikuwa mzuri kwa rapper wa Mwanza Fid Q ambaye alifanikiwa kushinda tuzo mbili za hip hop katika kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 (KTMA2014).

Ushindi wa Fid Q uliibua shangwe kubwa katika tuzo hizo kwa watu waliokuwa ukumbini huenda ni kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kubeba tuzo hizo ukiacha ile tuzo kushirikiana waliowahi kushinda Jay Mo, Fid Q na JCB (Ukisikia Paa).




Fid alishinda tuzo ya Msanii bora wa hip hop na mtunzi bora wa mashairi- hip hop.

Suma G ni mmoja kati ya rappers wakongwe katika game la hip hop, yeye ameiambia tovuti ya Times Fm mtazamo wake kuhusu ushindi wa Fid Q.

“Fid alikuwa anastahili kuchukua tuzo muda mrefu tu tukizungumza ule ukweli lakini sasa nadhani labda huu ndio muda wake muafaka ndio umefika ndio maana amepata hizo tuzo. Kwa sababu watu wengi sana walikuwa wanazungumza mpaka wengine wakawa wanaona kama vipi mchizi hata ajiondoe kwa sababu watu mtaani wanajua uwezo wake, wanajua Fid anafanya muziki wa kijamii zaidi.

“Kwa hiyo watu wanaoelewa wanaona mbona Fid anafanya muda mrefu lakini tuzo wanapewa watu wengine ambao labda hawapo kama Fid? Lakini kitu chochote kinahitaji subira ndio maana Fid alikuwa yupo kimya akaendelea kufanya na kweli muda umefika amepata. Na kweli muda umefika amepata, kwa hiyo nimpe pongezi Fid Q na nimuombee Mungu aendelee kufanya vizuri kwa sababu yeye ana mchango mkubwa sana kwenye game ya hip hop ya Tanzania na dunia nzima.”

Suma G ambaye ni member wa Hot Pot Family, ameachi wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muulize Meneja’ aliomshirikisha Profesa Jay. Endelea kufuatilia tovuti hii na sikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm leo kuanzia saa mbili kumili hadi saa nne kamili utausikia kwa mara ya kwanza.



Source:TimesFm
Previous Post Next Post

Popular Items