Video: Mohammed Dewji afanya mahojiano na BBC kuhusu uwekezaji wa ndani

Mmiliki wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited Mohammed Dewji amefanya mahojiano na BBC kuhusu uwekezaji wa ndani ya nchi na jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi wa Tanzania unaongezeka kwa kiwango fulani na hivyo kampuni ya Mohammed Dewji pia ni moja kati ya makampuni yanayofaidika zaidi na ongezeko hilo.




“Nchi kwa ujumla inafanya vizuri sana, tumeendelea kukua kiuchumi kwa asilimia 7 na tuko kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakua haraka zaidi.” Amesema Mohammed Dewji.

Ameeleza kuwa kuna ongezeko la pato la Tanzania kutoka dola milioni 30 mwaka 1999 hadi dola bilioni 1.1 na kwamba hata kampuni yake inakua zaidi kwa kuwa watu wanavyozidi kuongeza pato ndivyo uwezo wao wa kununua bidhaa unavyoongezeka.

Amesema kuwa sasa hivi wanaendesha kampeni ya kununua vitu vya Tanzania ‘to buy Tanzanian’ na kwamba hiyo inawezekana zaidi endapo makampuni yatatoa bidhaa bora zaidi na kuweka bei inayomudu ushindani, watanzania watanunua zaidi bidhaa za kwao.

Ameongelea pia kuhusu umoja wa nchi za Afrika Mashariki na kueleza kuwa kiuchumi utasaidia sana lakini watanzania wengi walikuwa bado wanauoga kuhusu kiwango cha watanzania ambao wamepata elimu kwa kulinganisha na nchi nyingine wanachama.

Bofya hapa kuangalia video: http://www.bbc.com/news/world-africa-26692518
Previous Post Next Post